We use cookies to personalise content and ads, to provide social media features and to analyse our traffic. Read more…
Friday
06
APR

Kongamano La Kiswahili Duniani Miaki 50 Ijayo - MS TCDC

07:30
02:30
MS TCDC
Event organized by MS TCDC

Get Directions

Category
#var:page_name# cover

Chuo cha MS-TCDC kinaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1967, tarehe 6 na 7 Aprili, 2018 Usa – River, Arusha Tanzania.

Katika maadhimisho haya Idara ya Kiswahili na Utamaduni itakuwa inasherehekea kuwepo kwake tangu kuanziswa chuo hiki. Kwa hali hiyo idara imepanga kushirikisha wadau mbalimbali wa ufundishaji Lugha ya Kiswahili na Utamaduni kwa wageni ili kushirikishana mafanikio, pamoja na kutafakari mustakabali wa Lugha ya Kiswahili duniani kwa miaka 50 ijayo.

Hivyo basi, maadhimisho haya ni fursa kwa wapenzi na wadau wa Kiswahili, wakufunzi wa vyuo, wanafunzi wa vyuo vikuu, watafiti, wasanii, waandishi wa habari, wachapishaji na wakuza mitaala kukutana na kushirikishana mafanikio ya Chuo cha MS TCDC kwa miaka 50 na kutafakari pamoja mustakabali wa Lugha ya Kiswahili duniani katika miaka 50 ijayo.

Hivyo basi tunakaribisha makala mbalimbali katika mada zifuatazo:-

Ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni
Maendeleo ya Kiswahili na utangamano wa Afrika kwa jumla
Kiswahili kama Lugha mojawapo nyeti duniani
Kiswahili ni nyenzo na hazina ya maendeleo endelevu duniani
Nafasi ya Taasisi za Lugha ya Kiswahili katika Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Nafasi ya Kiswahili katika taaluma nyingine za kitaalamu
Uhifadhi wa Fasihi Simulizi ya Kiswahili
Lugha ya Kiswahili na Vyombo vya Habari
Mchango wa wataalamu wa Kiswahili katika uhifadhi wa lugha ya Kiswahili na makavazi za kiutamaduni
Ufundishaji wa Kiswahili kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa

Kwa washiriki wasio wasilisha Makala: Unaweza kishiriki Kongamano hili bila kuwasilisha makala, tafadhali thibitisha ushiriki wako kabla ya tarehe 31 Machi 2018 kwa kujaza fomu ya kuhudhuria kwa kujaza fomu yakushiri hapa au kutuma barua pepe kwa mratibu wa maadhimisho kiwelub@mstcdc.or.tz Au piga simu namba + 255 713 727806 au +255 754 693260 kwa maelezo zaidi.

Karibuni Sana

MS TCDC

Venue

MS TCDC